Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama chaShirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadr al-Din al-Qubanchi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za swala ya Ijumaa alizozitoa katika Husseinia Kuu ya Fatimiya ya Najaf Ashraf, alisema: Janga la Lebanon limefichua unyama wa Kizayuni, na hapa tunatoa pole na kuonesha masikitiko yetu kwa watu wa Lebanon, hasa Mashia wa Lebanon, na tunawaambia kwamba; sisi tuko pamoja nanyi, basi vumilieni na muwe na subira:
(فعسی الله أن یأتی بالفتح أو أمر من عنده)
“Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo kutoka Kwake.”
Aliongeza kuwa: Unyama huu wa Uzayuni unatukumbusha maneno ya Imamu Husayn (as) siku ya Ashura liliposhambuliwa hema, aliposema:
(أنا الذی أقاتلکم وتقاتلوننی والنساء لیس علیهن جِنَاح)
“Mimi ndiye ninayepigana nanyi na ninyi mnayepigana nami, na wanawake hawana hatia katika jambo hili.”
Leo Uzayuni, baada ya kushindwa kuiangamiza Hizbullah, unavamia nyumba na familia.
Walitaka kuiangusha Iran, ikageuka kuwa nguvu kubwa
Katika sehemu nyingine ya khutba alisema: Nani mshindi wa mapambano haya? Jibu ni kwamba hatimaye haki imeshinda. Walitaka kuiangusha Iran, ikawa nguvu kubwa; walitaka kuvunja umoja, watu wa Iran wakaungana; walitaka kuitenga dini, dini ikawa kiongozi wa barabara za Iran, na kauli mbiu yao ilikuwa “usiogope, usihuzunike” na “Hayhaat minna al-dhillah”.
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf pia katika muktadha huu aliishukuru Iran kwa kuruhusu kupita kwa meli za mafuta za Iraq.
Khatibu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf katika sehemu ya khutba ya kidini, baada ya kuusia uchamungu na kuashiria kumbukumbu ya mwaka ya shahada ya Imamu Sadiq (as), alisema: Imani ina hatua mbili; hatua ya kwanza ni uongofu na ya pili ni uthabiti.
Akanukuu aya isemayo:
(اللهُ یَدْعُو إِلَیٰ دَارِ السَّلَامِ وَیَهْدِی مَن یَشَاءُ إِلَیٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِیمٍ)
na aya:
(یُثَبِّتُ اللهُ الَّذِینَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ)
“Mwenyezi Mungu analingana kwenye makazi ya amani, utulivu na salama, na humwongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka” na “Mwenyezi Mungu huwathibitisha walioamini kwa neno thabiti.”
Leo sisi tuko katika hatua ya uthabiti, na hapa ndipo tunaomba: «اللهم ثبتنی علی الهدی ما أحییتنی ولا تزغ قلبی بعد إذ هَدَیتنی». Hii ndiyo dua ambayo Imamu Sadiq (as) alimfundisha mmoja wa wafuasi wake kwa ajili ya uthabiti wa imani: «رَضیتُ بالله ربّاً وبالإسلام دیناً و بمحمد نبیاً و بعلی إماماً و بالأئمة من بعده».
Shahidi Imamu Khamenei ni mwanzilishi wa nadharia ya mhimili wa muqawama na mwanzilishi wa nadharia ya jihadi ya ufafanuzi
Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadr al-Din al-Qubanchi pia aligusia siku ya arobaini ya shahada ya Imamu Khamenei na kusema: Shahidi Imamu Khamenei ni shakhsia aliyeliongoza kwa mafanikio Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran kwa muda wa miaka 37, na yeye ni mfafanuzi wa nadharia ya mhimili wa muqawama na pia mwanzilishi wa nadharia ya jihadi ya ufafanuzi.
Katika suala la mhimili wa muqawama na umoja wa waumini, alirejea aya isemayo:
(قَاتِلُوا الْمُشْرِکِینَ کَافَّةً کَمَا یُقَاتِلُونَکُمْ کَافَّةً)
“Piganeni na washirikina wote kama wao wanavyopigana nanyi nyote,”
na kuhusu jihadi ya ufafanuzi akanukuu aya:
(إِن جَاءَکُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَیَّنُوا)
“Iwapo fasiki atawaletea habari, basi ichunguzeni,”
na akaeleza kwamba Shahidi Imamu Khamenei ameona ufafanuzi kuwa ni jukumu la waumini wote ili watu wasiangukie katika mitego ya vyombo vya habari vinavyopotosha.
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf pia alisema kwamba Imamu Khomeini aliwasilisha miradi miwili; mradi wa harakati ya umma wa Kiislamu na mradi wa kueneza Mapinduzi ya Kiislamu, na baada ya Imamu marehemu, Shahidi Imamu Khamenei aliweka msingi wa nadharia ya mhimili wa muqawama na nadharia ya jihadi ya ufafanuzi.
Kuhusu shakhsia ya Shahidi Imamu Khamenei, alimwelezea kuwa ni kielelezo cha subira, ujasiri, fiqhi, siasa, dini na tawakkul.
Shahidi Sadr ni mwanzilishi wa mapambano ya kielimu ya Kiislamu dhidi ya fikra za kimada za kisasa
Khatibu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf katika kumbukumbu ya mwaka ya shahada ya Shahidi Sadr wa kwanza alisema: Shahidi Sayyid Sadr, mbali na nafasi yake ya kifiqhi na marja’iyya, alikuwa mwanzilishi wa mapambano ya kielimu ya Kiislamu dhidi ya fikra potofu za kisasa, na vitabu vya “Falsafatuna” na “Iqtisaduna” vilikuwa katika mstari wa mbele wa njia hii. Pia alikuwa mwanzilishi wa jukumu la wanazuoni katika medani ya kijamii.
Maoni yako